- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WANANCHI MKOA WA MANYARA WANUFAIKA NA MRADI WA MIVARF
MANYARA: Serikali imeendelea kuwainua wananchi kiuchumi nchini kupitia mradi wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) unaolenga hususan maeneo ya vijijini.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) alisema kuwa Serikali kupitia mradi huo imefanya kazi kubwa sana kwa kuboresha miundombinu ya masoko na huduma za kifedha kwa wakulima na wananchi maskini.
Mradi huu umekuwa na faida nyingi sana ikiwemo kuongeza thamani ya mazao kutokana na ujenzi wa magala ya kuifadhia mazao, miundombinu ya barabara ambayo imewezesha usafirishaji wa mazao kwenda kwenye soko kiurahisi na hivyo thamani ya mazao hayo itaongezeka na huduma za kifedha zimeweza kuwa karibu na wananchi wanauwezo wa kutunza fedha zao benki na vilevile kupata mikopo.
“Mradi huu ukawe wa mfano na wananchi wahakikishe unakuwa endelevu kwa kutunza vizuri maghala, masoko, mashine na miundombinu, kwa kufanya hivyo hii miradi itaendelea kudumu na itaendelea kutoa huduma iliyokusudiwa na uchumi wa mwananchi kukua” alisisitiza Mhagama.
Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana wa kijiji cha Magugu kuchangamkia fursa zilizopo nchini kwa kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyoweza kuwa kwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mbunge la Babati Vijijini, Mhe. Vrajil Jituson amesema kuwa wakazi wa vijiji vya Maswale, Magugu n.k wamenufaika na mradi huo kwa kutengenezewa barabara, madaraja na magala ya mazao ambayo yamewasaidia wananchi kukua kiuchumi na upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii.
“Mradi wa MIVARF umeinua hali ya uchumi vijijini ambapo kijiji cha Matufa, Masware, Kichameda na Magugu vimenufaika. Kwani kwa sasa wakazi wa vijiji hivyo wameweza kujiajiri kwenye kilimo cha mpunga kutokana na uwepo wa miundombinu ya uhakika” alisema Kaaya
Aidha, Afisa Kiungo Mradi wa MIVARF Manyara, Bi. Lulu Kaaya ameeleza kuwa ujenzi wa miundombinu na ghala kumefanya wakazi wa maeneo haya kuanzisha vikundi mbalimbali vya kilimo ikiwemo kikundi cha AMCOS ambao wamekuwa wakilima mpunga kwa sehemu kubwa kutokana na thamani ya mazao imeongezeka na tunauhakika wa sehemu ya kuyatunza.