- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WANAJESHI WA NIGERIA WAMUUA MFUASI MMOJA WA SHEIKH ZAKZAKY
Wanajeshi wa Nigeria wamuua mfuasi wa Sheikh Zakzaky
Wanajeshi wa serikali ya Nigeria wamewashambulia wafanya maandamano wanaotaka kuachiwa huru Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky na kumuua mtu mmoja.
Mfuasi huyo wa Sheikh Zakzaky aliuawa jana katika jimbo la Kaduna kaskazini magharibi mwa Nigeria katika maandamano ya wafuasi wa kiongozi huyo wa Kiislamu yaliyofanywa katika maeneo zaidi ya 50. Wafanya maandamano hayo wamemtaka Rais Muhammadu Buhari amwachie huru kiongozi huyo wa Waislamu wa Kishia. Itakumbukwa kuwa kabla ya maandamano hayo, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilikuwa imemuomba Rais Buhari amuachie huru Shekh Zakzaky ili aweze kupatiwa matibabu kufuatia maradhi yanayomkabili ya kupooza aliyopata hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa na Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imeeleza kuwa imethibitika kuwa hali ya kiafya ya Sheikh Zakzaky ilikuwa mbaya siku mbili zilizopita na kwamba anahitaji msaada wa haraka wa kitiba. Taarifa hiyo imeongeza kuwa inavyoonekana ni kuwa wale wanaomshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky wanapoteza tu muda ili wamuuwe.