Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 12:46 am

NEWS : WANAFUNZI WA IRAN WAAHIDI KUTEKELEZA AZMA YAO YA KIFO KWA MAREKENI NA ISRAEL

Wanafunzi wa Iran waahidi kuendeleza nara ya 'Kifo kwa Marekani, Kifo kwa Israel'

Wanafunzi wa Iran waahidi kuendeleza nara ya 'Kifo kwa Marekani, Kifo kwa Israel'

Jumuiya za wanafunzi nchini zimetangaza katika marasimu ya leo tarehe 4 Aban katika eneo kulipokuwa ubalozi wa zamani wa Marekani maarufu kwa jina la 'Chaka la Ujasusi la Marekani mjini Tehran' kwamba wataendeleza nara ya 'Kifo kwa Marekani na kifo kwa Israel.'

Marasimu ya tarehe 13 Aban yameanza asubuhi ya leo mjini Tehran na katika miji tofauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuhudhuriwa na wananchi, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari vyuo vikuu na viongozi wa serikali. Tarehe 13 Aban sawa na tarehe Nne Novemba 2017 inatambuliwa kama siku ya kitaifa ya 'Kupambana na Uistikbari' nchini Iran.

Siku ambayo ubalozi wa Marekani ulipodhibitiwa na wanafunzi wa Iran mjini Tehran

Katika sherehe hizo jumuiya za wanafunzi zimetoa taarifa zikisema kuwa, matukio ya mapinduzi ya Kiislamu, kama vile kubaidishwa Imam Khomein (MA) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenda nchini Uturuki hapo mwaka 1964, mauaji ya wanafunzi yaliyofanywa na utawala kibaraka wa Shah hapo tarehe nne Novemba 1978 na kadhalika kudhibitiwa ubalozi wa zamani wa Marekani nchini Iran (pango la ujasusi la Marekani) hapo tarehe nne Novemba mwaka 1979, ni matukio yaliyobakia katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini hapa. Ripoti hiyo sambamba na kubainisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa mstari wa mbele katika kutetea usalama wa dunia na kuwa na mahusiano mema na mataifa yote yanayopenda amani na uhuru, imesema kuwa, uistikbari wa dunia ambao unaongozwa na shetani mkubwa (yaani Marekani) unatekeleza ukatili na jinai kubwa dhidi ya watu wa mataifa yanayodhulumiwa duniani.

Wanafunzi na wananchi wa Iran wakitoa nara ya 'Kifo kwa Marekani, Kifo kwa Israel'

Aidha ripoti hiyo sambamba na kusisitiza kwamba Marekani na utawala haramu wa Kizayuni kwa kushirikiana na baadhi ya madola katika eneo la Mashariki ya Kati, zinapora raslimali za ulimwengu wa Kiislamu, kwa mara nyingine imetangaza kuenzi na kufuata ushauri wa Imam Khomein (MA) na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Pia jumuiya hizo za wanafunzi wa Iran zimetoa ujumbe kwa Rais Donald Trump wa Marekani kwamba, anatakiwa kufahamu kuwa eneo la Ghuba ya Uajemi litaendelea kuitwa Ghuba ya Uajemi daima.