Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 8:44 pm

NEWS : WAMAREKANI SASA WAANZA KUCHOSHWA NA DONALD TRUMP

Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, umaarufu wa rais wa Marekani Donald Trump umeporomoka mno.

Uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na televisheni ya NBC pamoja na gazeti la Wall Street Journal unaonesha kuwa asilimia 58 ya wananchi wa Marekani wanachukizwa na vitendo na utendaji wa Trump kama rais wa nchi yao.

Maandamano ya kumpinga Trump nchini Marekani

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kiwango cha kukubalika rais wa Marekani Donald Trump kimepungua kwa asilimia 38, na hicho ni kiwango cha chini kabisa cha kutoridhishwa na utendaji wa Trump hadi hivi sasa.

Itakumbukwa kuwa umaarufu wa Trump mwezi Septemba mwaka huu ulikuwa kwa asilimia 43 kati ya wananchi wa Marekani.

Upayukaji na kutoa maneno yanayozusha makelele mengi, kuyaunga mkono magenge yenye misimamo mikali ya ubaguzi wa rangi, siasa zaka za kupinga wageni na kushindwa kwake kuweka mpango wa matibabu Wa kushika nafasi ya bima ya afya ya Obama aliyoifuta ni miongoni mwa mambo yaliyoporomosha vibaya umaarufu wa Trump ndani ya Marekani kipindi kifupi tu cha hivi karibuni.