Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 9:49 am

NEWS: WALIOHUSIKA NA UVUJISHAJI WA MITIHANI DOM WAVULIWA MADARAKA.

DODOMA: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Dk Binilithi Mahenge ametangaza kuwavua Madaraka waratibu Elimu wa kata na walimu wakuu waliobainika wazi wazi katika tuhuma za uvujishaji wa mitihani katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.


Mbali na hilo mkuu huyo amesema kuwa wapo walimu wanne ambao walikuwa wasimamizi wa mitihani katika shule binafsi ya Kondoa nao wamesimamishwa Kazi kwa lengo la kupisha uchunguzi.


Katika hatua huyo Mhandisi Mahenge ameziagiza mamlaka za nidhamu kuwafungulia mashitaka wale wote ambao wamehusika na tuhuma hizo na kuwataka kusimamia kwa ukamilifu marudio ya mitihani huyo.

Amesema kamati za mitihani za mkoa na wilaya husika ziendelea kufanya uchunguzi wa kina ili yoyote atakayebainika achukuliwe hatua stahiki na kwamba mkoa hauna mzaha na hatua huyo na atakayebainika atapata taabu sana.

Mhandisi Mahenge amebainisha wazi kuwa jumla ya shule za msingi 103 katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma zimefutiwa mitihani ya darasa la kutokana kutokana na udanganyifu na wizi wa mitihani.


Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa Mhandisi Binilith Mahenge amesema kitendo kilichofanywa na watumishi wa sekta ya Elimu ni aibu kwa mkoa wa Dodoma.


Kutokana na hali hiyo Mhandisi Mahenge amewataka watumishi wote kuhakikisha wanafanya Kazi kwa maadili ili kufanikisha Kazi ambayo wanaifanya.


Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kamati ya Mkoa ikiongozwa na RAS imetekele wa wajibu wake wa kulinda na kugawa mitihani kwa uadilifu mkubwa.


Kati ya shule ya binasi iliyohusika na wizi wa mitihani ni pamoja na shule ya msingi Integrity .