Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:44 am

NEWS: WALIMU SABA WATIMULIWA KAZINI KWA UTORO TABAORA

Tabora: Walimu saba kutoko katika shule tofauti za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali likiwemonkubwa la utoro kazini.

Akiongea na waandishi wa habari juzi Sept. 28 Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wilaya ya Igunga, Hamisi Mpume, aliwataja walimu hao kuwa ni pamoja na Paul Msabila aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Igunga mjini, Mary Elvance Kesi aliyekuwa akifundisha Shule ya Msingi Bulunde.

Wengine ni Lazaro Cheyo wa Shule ya Sekondari Nguvumoja, Leonard Chakupewa wa Shule ya Msingi Ziba, Rogasian Pacho wa Shule ya Msingi Nyandekwa, Sostenes Chiboko wa Shule ya Sekondari ya Sungwizi na Faustine Obadia wa Shule ya Msingi Ziba.

Mpume alisema kuwa walimu hao walifikishwa katika tume ya utumishi wa walimu ya Wilaya ya Igunga na kubainika kuwa na makosa mbalimbali yakiwamo utovu wa nidhamu na utoro kazini kwa muda mrefu pasipo taarifa yoyote kwa mwajiri wao.

Mpume alisema pia wapo baadhi ya walimu ambao hakuweza kuwataja majina ingawa ameshapewa barua za onyo baada yakubaini makosa yao siyo yakufukuzwa kazi.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, ambaye pia ni Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Ntulila Hadoni, alisistiza taratibu zote za utumishi zimezingatiwa kabla ya kuchukuliwa uamuzi huo kwa mujibu wa sheria.