Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:46 pm

NEWS: WALEMAVU WALIA NA MKURUNGEZI WA HALMASHAURI.

SINGIDA: Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu mkoa wa Singida (SHIVYAWATA) limeitaka ofisi ya mkurugenzi Wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni kuendelea kuwa chachu ya kuwasaidia watu wenye ulemavu ili kuondokana na changamoto walizo nazo.

Rai hiyo imetolewa na Iddy Kingugu katibu Shivyawata mkoa wa Singida wakati wa mkutano maalum wa walemavu uliofanyika wilaya ya Manyoni mjini hapa.

Katibu huyo amesema walemavu wa ngozi (Albino) wamekuwa na changamoto nyingi huku adui mkubwa akiwa ni miale ya jua ambayo imekuwa ikiwasababisha kansa ya ngozi

Awali akifungua mkutano huo mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Charles Fussi, amesema serikali inatambua mchango wa kundi hilo nakusema wanahitaji kupatiwa mahitaji muhimu kama watu wengine ikiwa ni pamoja na kuthaminiwa.

Aidha katika upande wa kiliniki ya ngozi mkurugenzi huyo amesema katika kuwasaidia walemavu wa ngozi halmashauri imepokea changamoto hizo hivyo amewaomba viongozi wa shirikisho hilo kupanga siku watakazo hudhuria kiliniki, na halmashauri itagharamia gharama hizo

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amewataka walemavu hao kupendana wao kwa wao na kuachana na chuki na majungu hukuakisisitiza upendo uanzie nakusema, kwakufanya hivyo itawasaidia kusongambele.

Nae kaimu katibu tawala Laila Sawe amewasisitiza walemavu kuhakikisha wanajitahidi katika kufanya kazi pamoja na ulemavu walionao ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.