- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA WACHANGIA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.
DODOMA: Serikali imesema Wakulima wamechangia kwa kiasi kikubwa, kuimarika kwa uchumi nchini, ambapo mpaka kufikia Novemba mwaka huu uchumi ulikuwa umefikia asilimia 6.8.
Hali hiyo inaelezwa katika ripoti ya Shirika la Fedha duniani (IMF) ambayo serikali imeizungumzia kupitia kwa Msemaji wake mkuu na ambaye ni Mkurugenzi Wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan Abas.
Abas amesema hali ya uchumi inaridhisha kwa sasa ambapo imeonekana mageuzi makubwa ya kuongezaka kwa makusanyo hadi kufikia trilioni 14 Novemba mwaka huu.
Aidha amesema serikali imetenga kiasi cha fedha tsh bilioni 20 kwa ajili ya kulipa madeni ikiwemo kulipa madeni ya walimu.
Pamoja na hayo amesema serikali imelipa trilion 1.3 kwajili yakuwalipa madeni ya wastaafu na tsh bilioni 900 zililipwa kwa ajili ya madeni ya nje na ndani ya Taifa.
Mbali na hayo amesema misingi ya Sera inatekelezwa ili kusaidia kuboresha utekelezaji Wa ushauri Wa taalamu Wa kiuchumi ,kushusha mfumuko Wa bei, ulipaji Wa madeni, uwezo Wa kuhifadhi fedha za kigeni na kusimamia ukusanyaji Wa mapato na kuthibiti matumizi holela ya fedha.
Hata hivyo amesema sheria ya takwimu kuzingatiwa katika kutoa taarifa na kwamba serikali haitaruhusu mtu yeyote kuharibu uchumi wanchi kwa mihemko ya kisiasa au binafsi.
Pia ameongeza kuwa Uchumi wanchi yoyote ili ukuwe ni lazima usimamiwe kwa weledi zaidi na kuongeza kuwa hali ya uchumi nchini itaendelea kukua na kubadilisha mwelekeo wa maisha uliopo kwa kuzingatia mapato ya wananchi.
Katika hatua nyingine Dk Abbas alizitaja changamoto zilizojitokeza katika tathimini hiyo kuwa ni katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato, wanachi kukopa katika mabenki na kishindwa kurudisha, matumizi yasiyokuwa na tija kwa Taifa jambo ambalo serikali inaliangalia upya ikiwa ni pamoja na kubana matumizi katika safari za nje kwa watumishi wa serikali.
Pia amebainisha kuwa hatua iliyopo katika deni la taifa, Tanzania inafaa kuendelea kukopesheka na benki ya Dunia kutokana na kulipa jumla ya asilimia 34 za madeni