- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKUHUMIWA KUNYONGWA BAADA YA MAUWAJI YA WATU WENYE ULEAMAVU WA NGOZI
Watuhimiwa 34 wa kesi za mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia katika matukio 67 yaliyoripotiwa kwa kipindi cha miaka 11kuanzia 2006 hadi 2017 huku jamii ikitakiwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kufichua vitendo hivyo vya kikatili.
Matukio hayo yameonekana kujitokeza zaidi katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo yanahusishwa na imani za kishirikina katika kutaka kuonzeza uzalishaji kwenye madini, uvuvi, kupata mazao mengi na kutafuta vyeo.
Beatrice Mpembo ni wakili wa serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP akitoa taarifa hiyo amesema changamoto wayokutana nayo ni majalada ya kesi kutokuandikwa kuwa ni mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
Kwa upande wake muwakilishi kutoka katika jeshi la polisi mrakibu mwandamizi Ralph Meela wakati akitoa mada katika mkutano wa wa kujadili mwaswala ya watu wenye ulemavi wa ngozi amesema matukio hayo mwanzoni yalikuwa yakichukuliwa kama mauwaji mengine bila kuhusiaha imani za kishirikina na siasa.
Bahame Nyandugu ni mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu ambao amesema lengo lao ni kutoka na mikakati ya pamoja ya kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kabisa.
Nao watu wenye ulemavu wa ngozi wameitaka serikali kuongeza kasi ya utoaji wa elimu katika mikoa yote bila kujali maeneo ambayo mauwaji hayo hujitokeza mara kwa mara.
Mikoa inayoongoza kwa mauwaji ya walemavu wa ngozi ni Mwanza Kagera na Geita huku yakijitokeza katika mikoa zaidi ya 17 tangu mwaka 2006 hadi sasa.