- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKAZI 300,000 JAPAN WAHAMISHWA KUTOKANA NA DHURUBA KALI
Serekali ya Japan imewahamisha wakazi karibu 300,000 na kufutwa kwa safari za ndege mia moja wakati dhoruba kali inayofahamika kwa jina la Jebi ikitarajia kupiga katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo leo Jumanne.
Jebi ni dhoruba kali zaidi ambayo imekua ikikumba Japan tangu mwanzoni mwa majira ya joto, wakati katika miezi ya hivi karibuni nchi hiyo ilikumbwa na majanga mengi ya asili kama vile mvua yenye upepo mkali, vimbunga, maporomoko ya ardhi, mafuriko na joto kali - ambavyo vilisababisha mamia ya watu kupoteza maisha.Mamlaka ya Japan imetoa maelekezo ya kuhamishwa kwa wakazi karibu 300,000 na kufutwa kwa safari za ndege zaidi mia moja wakati dhoruba kali inayofahamika kwa jina la Jebi ikitarajia kupiga katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo leo Jumanne.
Dhoruba hii inatarajiwa kuanza kupiga huko Shikoku, kisiwa kidogo kati ya visiwa vinne vikuu nchini Japan, kabla ya kupiga Honshu, kisiwa kikuu, huko Osaka, kisiwa cha pili kwa ukubwa nchini humo.
Mamlaka imewataka watu 280,000 kuhama makaazi yao, wakati upepo na mvua zimeanza kujikusanya.
Safari za ndege karibu 600 zimeutwa, ikiwa ni pamoja na safari za majini, televisheni ya serikali NHK imeripoti.
Mji mkuu, Tokyo, hautokubwa na dhoruba hii lakini kunatarajiwa kunyesha mvua kubwa na upepo mkali mwishoni Jumanne jioni.