- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WAKATI MWAKA MPYA UKIINGIA WANNE WAFARIKI DUNIA HUKO LONDON
Sambamba na kuanza mwaka mpya, watu wanne wauawa kwa silaha baridi katika viunga vya London
Polisi ya London imetangaza kuwa sambamba na kuanza mwaka mpya wa 2018 kumesajiliwa mashambulizi kadhaa ya silaha baridi katika mji huo mkuu wa Uingereza.
Taarifa ya polisi ya London imesema kuwa, watu wanne wameuawa katika mashambulizi tofauti ya kutumia silaha baridi katika maeneo mbalimbali ya mji huo na wengine kadhaa wamejeruhiwa sambamba na kuanza mwaka mpya wa 2018. Hali ya majeruhi mmoja inaripotiwa kuwa mbaya.
Polisi ya Uingereza haikutoa maelezo kuhusu sababu ya mashambulizi hayo na iwapo yamefanyika kwa sababu za kigaidi au la.
Taarifa ya Polisi ya London imesema kuwa, katika mwaka uliomalizika wa 2017 karibu watu 80 waliuawa katika mashambulizi ya silaha baridi mjini London pekee na kwamba wengi wao walikuwa vijana waliokuwa na umri wa chini ya miaka 25.
Idadi ya jinai na mauaji ya kutumia silaha baridi mjini London imekuwa ikipanda na kuongeza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.