- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAITARA ASEMA NIMARUFUKU MZAZI KUCHANGISHWA MICHANGO
NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara ametilia mkazo Agizo la Rais Magufuli la marufuku ya wazazi kuchangishwa michango ya wananfunzi shuleni huku akisema utaratibu huo ubaki pale pale na kwamba, walimu wasithubutu kukiuka agizo hilo.
Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametamka hayo wakati wa ziara ya kushukuru wananchi wa jimbo lake waliopo kwenye Kata ya Chanika ikiwa ni baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge Ijumaa iliyopita.
Akiwa kwenye ziara hiyo jimboni kwake Waitara amesema, utaratibu wa kuwaandikisha watoto wote waliofika uamri wa kwenda shule katika elimu ya awali na msingi unapaswa kutekelezwa kwa kuwa ndio sheria inavyoelekeza.
Mbunge huyo ambaye awali alitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewaeleza wakati wa Chanika kuwa, ataendelea na oparesheni ya kuhakikisha wanafunzi wanaandikishwa shule huku akiahidi kuwa, wataothubutu kukwamisha utekelezwaji wa agizo hilo kutokana na michango atakiona.
“Nasimamia kwa karibu suala la elimu, michango yenye kero imeondolewa, watoto darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza waandikishwe, hii ni oparesheni ya kuhakikisha wanaandikishwa.
“Ni marufuku kuzuia mwanafunzi kujiunga darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza kama mzazi wake hajatoa michango, ukizuiliwa kuandikisha mtoto sababu hujatoa mchango toa taarifa,” amesema Waitara.
Amesema Serikali inakataza michango yenye kero hivyo atakayezuia watoto kuandikishwa kwa sababu hiyo atachukuliwa hatua