Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 5:52 am

NEWS : WAISLAMU NIGERIA WAZIKA WALIOUAWA KATIKA AROBAINI YA IMAM HUSSEIN

Waislamu wa Nigeria wawazika mashahidi waliouawa na polisi karika Arubaini ya Imam Hussein (as)

Waislamu wa Nigeria wawazika mashahidi waliouawa na polisi karika Arubaini ya Imam Hussein (as)

Miili ya mashahidi wa shambulizi la jeshi la Nigeria dhidi ya washiriki wa marasimu ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as) imefanyiwa mazishi na Waislamu wenzao nchini humo.

Wakazi wa mji wa Kano nchini Nigeria Jumapili ya jana walishiriki kwa wingi katika mazishi ya mashahidi wanne waliouawa na askari wa serikali wakati walipokuwa katika kumbukumbu za Arubaini ya mjukuu wa Mtume (saw) al-Imamul-Hussein (as).

Harakati za amani zilizokuwa zikifanywa na Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky

Mashahidi hao waliuawa kwa kupigwa risasi moja kwa moja na maafisa usalama wa serikali mjini Abuja, mji mkuu wa Nigeria ambapo katika hujuma hiyo ya kinyama ya jeshi la serikali makumi ya watu wengine walijeruhiwa. Duru za habari zimearifu kwamba, polisi ya Nigeria iliwatia nguvuni Waislamu wengi waliokuwa wakishiriki marasimu hayo ya amani ya Arubaini na kwenda nao kusikojulikana. Wimbi la ukandamizaji wa kuchupa mpaka dhidi ya Waislamu nchini Nigeria lilianza mwezi Disemba mwaka 2015, baada ya jeshi la nchi hiyo kuvamia Husseinia ya mji wa Zaria katika jimbo la Kaduna.

Mashambulizi ya jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu wasio na hatia wa Shia nchini humo

Katika uvamizi huo, mamia ya watu wakiwemo watoto watatu wa Sheikh Ibrahim Yaqoub El Zakzaky, Kiongozi wa Waislamu wa Kishia wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika waliuawa sambamba na kutiwa mbaroni yeye na mke wake na kupelekwa kusikojulikana. Saudia inatajwa kuhusika na ukandamizaji wanaokabiliwa nao Waislamu hao wa Shia, kufuatia kutuma viongozi wengi wa Kiwahabi ndani ya taifa hilo kwa lengo la kueneza misimamo ya chuki na ukufurishaji dhidi ya watu wengine.