- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : WAINGEREZA WALIVYOTUMIA GHARAMA KUBWA KWENYE HARUSI YA MWANAMFALME JANA
Wananchi wa Uingereza wameghadhabishwa mno na gharama kubwa za harusi ya Mwanafalme wa nchi hiyo, Harry na muigizaji wa Marekani, Meghan Markle iliyofanyika jana Jumamosi.
Utafiti wa maoni uliofanywa na tovuti ya YouGov umebainisha kuwa, asilimia 57 ya Waingereza walitaka familia ya Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza ilipie gharama za harusi hiyo ya kifahari.
Hata hivyo harusi hiyo ambayo ilihudhuriwa na takriban watu 2000 katika Kasri ya Windsor, yapata kilomita 32 magharibi mwa mji mkuu London, iligharamiwa na fedha za walipa kodi.
Tovuti za biashara za Bridebook na Business Insider zimesema harusi hiyo ya kifalme iligharimu dola milioni 45 za Marekani (pauni milioni 32), fedha zilizochotwa kutoka kwenye hazina ya serikali.
Ijumaa iliyopita, siku moja kabla ya harusi hiyo, mamia ya wananchi wa Uingereza walifanya maandamano nje kidogo ya mji wa London kulalamikia gharama hizo za harusi, katika hali ambayo wananchi wengi wa Uingereza hawana makazi.
Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya watu wasio na makazi nchini Uingereza imeongezeka kwa asilimia 134, tangu Chama cha Kihafidhina kiingie madarakani mwaka 2010.