Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 11:50 pm

NEWS : WAHAJIRI 900 WAOKOLEWA 7 WAPOTEZA MAISHA PWANI YA LIBYA

Wahajiri 900 waokolewa, 7 wafa maji katika pwani ya Libya

Wahajiri 900 waokolewa, 7 wafa maji katika pwani ya Libya

Miili saba ya wahajiri haramu imepatikana ndani ya boti ya plastiki karibu na pwani ya Libya, huku mamia ya wengine wakiokolewa kusini mwa bahari ya Mediterranean.

Msemaji wa Gadi ya Pwani ya Italia amesema miili hiyo ilipatikana jana Jumatano, wakati timu yake ya waokoaji ilipokuwa katika operesheni ya kuwanusuru wahamiaji haramu 900, kusini mwa bahari ya Mediterranean, wakiwa ndani ya boti hafifu za plastiki wakielekea barani Ulaya.

Hata hivyo afisa huyo ambaye ameongea na shirika la habari la Reuters hajatoa maelezo ya kina kuhusu uraia wa wahajiri hao au namna walivyokufa.

Wahajiri wa Kiafrika wakiokolewa na mabaharia wa Italia

Mapema wiki hii, mabaharia wa Gadi ya Pwani ya Libya walifanikiwa kukamata boti mbili za plastiki zilizokuwa zimebeba wahajri karibu 300 kutoka eneo la chini ya jangwa la Sahara barani Afrika, mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, wakiwa katika safari hatari ya kuelekea barani Ulaya kutafuta maisha.

Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imeitaka jamii ya kimataifa ichukue hatua haraka iwezekanavyo kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoisibu Libya na kuwapokea wakimbizi zaidi.