- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFANYAKAZI SHIRIKA LA VIWANGO TBS WABURUZWA MAHAKAMANI
Maafisa wawili wa Shirika La Viwango Tanzania TBS Ambao ni Manunuzi Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, Mohamedx Mzingi na Mkuu wa Textile Leather wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa miwili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 977.
Akisoma hati mashtaka wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Aneth Mavika amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mmbando kuwa kati ya Julai 16 na 30, mwaka 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) washtakiwa walitenda kosa.
Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa hao kwa nafasi zao na wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni walitumia madaraka yao vibaya katika uthamini wa zabuni namba AE-054/2013/2014/HQ/G/02 Lot namba 01.
Wakili huyo aliendelea kudai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ambapo kwa makusudi walipendekeza kampuni ya Bajuka International (T) Ltd ambayo ilikuwa haina sifa kupewa zabuni ambayo haikuendana na matakwa ya kitaalam kama yalivyokuwa kwenye nyaraka za zabuni kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kutimiza majukumu