- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAFANYABIASHARA SABASABA WALALAMIKIA UONGOZI WA SOKO KUWAHAMISHIA ENEO LA DAMPO.
DOM: Zaidi ya Wafanyabiashara 400 wa Mbogamboga na Matunda katika Soko la sabasaba Jijini Dodoma wamelalamikia kitendo cha kutakiwa kuondoka katika eneo hilo na Uongozi wa Soko Kwa madai kuwa sehemu wanayofanyia biashara ni ndogo haiwatoshi na hivyo kusababisha msongamano.
Wakizungumza Muakilishi news katika Soko hilo wafanyabiashara hao wamesema kuwa uongozi wa Soko la sabasaba umekuwa ukiwasumbua hasa Katibu kwa kuwataka waondoke waende eneo la dampo ambalo wamedai ni chafu na ni hatari Kwa Afya zao.
Wamesema kuwa suala hilo limekuwa ni kero kwao kutokana na kushindwa kufanya biashara kwaasababu ya kuhamishwa kila kukicha na hivyo kupoteza wateja.
Aidha wameuomba Rais John Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani wana mikopo huku familia zao zinawategemea kutokana na biashara hizo lakini cha kushangaza wamekuwa wakiingizia Serikali mapato kwa kulipa ushuru.
Aidha Katibu Mkuu wa Soko la sabasaba Nyamsuka Nyamsuka amekanusha suala la kutaka kuhamishwa Kwa wafanyabiashara hao na kwamba wengi wao wamehama katika maeneo yao ya biashara kitendo ambacho kinaweza kusababisha kushuka kwa mapato ya Serikali yanayotokana na ushuru wa Soko hilo.
Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa awali wafanyabiashara hao walikuwa eneo la Dampo wao ndio waliowahamisha kule baada ya kuona eneo ni dogo na usalama wa Afya zao lakini kumekuwa na suala la kisiasa ambalo limekuwa likileta mkanganyiko kwa Wafanyabiashara hao.
Muakilishi ilijitihada za kumtafuta Mwenyekiti wa Soko la Sabasaba Bw Athumani Makole ili kuzungumzia suala hilo uhudi hilo zigonga mwamba.