- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WASHAURIWA KUSIAMAMIA MAPATO KWA WELEDI
DODOMA: Wabunge wameshauriwa kushirikiana vyema katika usimamizi wa mapato ili kuifanya bajeti kutekelezeka.
Kauli hiyo imetolewa leo na mtaalamu wa masuala ya bajeti ktoka wizara ya fedha na mipango Dk.Charles Mwamwaja.
Akitoa mada juu ya umuhimu wa kuwa na bajeti kwa wabunge wanaotokana na kamati mbalimbali Dk.Mwamwaja amesema njia pekee ya kuwa na bajeti inayotekelezeka ni wabunge kushirikiana katika kusimamia mapato.
Akitoa mada kwa wabunge hao alisema licha ya kuwa bajeti inaambataana na fedha ya wafadhili lakini mpaka sasa ni asilimia 11 ya bajeti ambayo ni tegemezi.
Hata hivyo Dk.Mwamwaja amesema ni jambo la muhimu kuwepo vya vyanzo vingi vya mapato kutoka ndani ili kuifanya bajeti kuweza kutekelezeka.
Nao wabunge wakichangia alisema serikali imetumwa ikishindwa kubainisha vipaumbele anbavyo inatakiwa kuendana na bajeti halisi.
Akichangia mbunge wa Rombo Josephu Selasini (Chadema) alisema serikli inatakiwa kuwa na vipaumbele muhimu wakati wa kuandaa bajeti.
Mbali na hivyo amesema ni muhimu zaidi kuwapatia wabunge na kuwajulisha vyanzo muhimu vya mapato kutoka ndani badala ya kutegemea zaidi fedha za wafadhili.