Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 1:33 am

NEWS: WABUNGE WALIA NA SERIKALI.

DODOMA: Wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanazania wameitaka serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutoa elimu kwa wabunge juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Waliyasema hayo jana wakati wa semina ya kuwajengea uwezo juu ya kufuatilia matumizi ya fedha ya serikali siku moja bala ya bunge kuanza iliyofanyika mjini hapa.

Aidha walilalamikia kushindwa kuibua na kuchangia hoja bungeni kwa madai kutokuwa na elimu juu ya masuala ya kimaendeleo.

Wakizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo juu ya kufuatilia matumizi ya fedha ya serikali baadhi ya wabunge akiwemo Salim Turki mbunge wa Mpendae ,Joseph Selasini mbunge wa Rombo na Selemani Bugara mbunge wa Kilwa walisema mumekuwa na uoga kwa baadhi ya wabunge kuhoji kutokana na kutokuwa na uelewa wa baadhi ya sekta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mafunzo hayo Janeth Mbene ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ileje aliwataka wabunge kuungana kwa pamoja ili kukomesha tatizo la uoga wa kuzungumza kwani wao ni wawakilishi wa wananchi katika majimbo yao

Akijibu hoja za wabunge hao mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni mkaguzi mkuu wa nje ofisi ya taifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali Deogratias Kirama amesema swala la wabunge kuogopa kuongea bungeni wanaweza kulimaliza wenyewe kwa kuzingatia kanuni za bunge ama kuzirekebisha.

Katika mkutano wa bunge unaoanza Nov 7 bunge linataraji kujadili na kupitisha miswada mbalimbali pamoja na kutumia mkutano huo kupokea taarifa za utekelezaji wa kamati zake katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/ 2018