- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE WAKEMEA HOJA ZA UKANDA
Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (CCM) aliyeingia bungeni humo tangu mwaka 1995, alionesha kukerwa na ukanda kujadiliwa ndani ya Bunge tangu mkutano huu wa tisa uanze.
Alisema kitendo cha kufananisha maendeleo anayoleta Rais John Magufuli kuwa anapendelea Kanda ya Ziwa si kauli nzuri. “Jana watu (wabunge) humu walitokwa mapovu kwa ukanda, sisi wabunge tuchuje maneno yetu kabla ya kuyatoa. Sasa Bunge linajadili ukanda tukitoka huko tutakuja kujadili ukabila, rangi na dini zetu.
Tusiwagawe wananchi kwa ukanda,” Ndassa alisema. …Tuungane kupigana vita ya uchumi, tuna maadui wengi, tumuunge mkono Rais kwenye vita hii ya uchumi. Spika naomba akisimama mbunge kuzungumzia ukanda una mamlaka ya kumshughulikia,” alisema mbunge huyo.
Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM) alitaka mbunge anayezungumzia ukanda azuiwe kwani anakwenda kinyume na Katiba ya nchi inayozuia ubaguzi na kugawa Watanzania. “Sijaridhika na mjadala wa ukanda, asiyeona kazi nzuri ya Rais Magufuli ni mgonjwa, analinda rasilimali za nchi, asipingwe,” alisema.
Hata hivyo, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi wa upinzani bungeni na ambaye wabunge wa chama chake tangu Bunge lianze wamekuwa wakimlaumu Rais Magufuli anapeleka maendeleo na kufanya ziara Kanda ya Ziwa na kutokwenda mikoa mingine naye alikiri kuzungumzia ukanda bungeni si jambo zuri.
“Nakubaliana na Ndassa kuzungumzia ukanda si vizuri lakini aangalie chanzo ni nini. Mbona miaka minne iliyopita hatujazungumza sasa kuna mambo yanafanyika si sawa na msiba utatuumbua,” alisema Mbowe.
Ukiacha ukanda, Mbunge Ndassa alimlaumu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akidai ana kiburi, hasikilizi ushauri wa wabunge hasa wa Kamati ya Bajeti na kusisitiza “Dk Mpango una ka arrogance fulani, wabunge wa CCM wanakuheshimu, lakini huisaidii Serikali na hata kukupata ni ngumu, simu za wabunge hupokei jitahidi kusikiliza ushauri.
Ipo siku mtakwama na wataalamu wenzako na mtatuomba tuwakwamue nasi tutasema hapana, wewe si msikivu kwa wabunge, badilika, sisi sote tupo hapa katika boti moja,” alimweleza.
Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe (CCM) alimlaumu Dk Mpango kuwa hasikilizi ushauri wa Kamati ya Bajeti na atamharibia Rais Magufuli mwaka 2020 huku akifafanua: Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba (CCM) alisema Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2018/2019 unaojadiliwa bungeni hauna tofauti na wa mwaka jana na mwaka juzi na unazungumzia kukusanya kodi bila kuongeza uzalishaji na haushirikishi sekta binafsi.
Spika Ndugai aliwataka wabunge wa CCM kufunguka mambo ya msingi katika kujadilli mpango huo ili kumsaidia Waziri Mpango kutokuwa na mpango mbovu wa maendeleo.