- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WABUNGE NCHINI KENYA WAGOMA KUMUONGEZEA MUDA RAIS KENYATTA
Nairobi: Zaidi ya Wabunge 40 wa bunge la Kenya, Jumatano jana walishindwa kupitisha muswada uliokusudiwa kuifanyia katiba marekebisho, kwa nia ya kubadilisha tarehe ya uchaguzi mkuu.
Hoja iliyokuwa imewasilishwa bungeni, ilitaka tarehe hiyo ibadilishwe kutoka mwezi Agosti, hadi mwezi Desemba ambayo ingemuwezesha Rais wa Sasa Uhuru Kenyatta kukaa madaraka kwa zaidi ya miezi 5.
Lakini muswada huo haukufua dafu baada ya kutopata idadi ya wajumbe inayo hitajika ili kuupigia kura.
Mapendekezo hayo yalikuwa yamewasilishwa na mbunge wa chama cha upinzani, Ford Kenya, Chris Wamalwa.
Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, akizungumza wakati wa kikao cha Jumatano, alisema muswada huo haungepigiwa kura kwa sababu haukuungwa mkono na wabunge wa kutosha kama inavyo takikana na katiba.
Baada ya hesabu ya waliokuwepo bungeni kufanywa, spika huyo alitangaza kwamba kulikuwa na wabunge 187 na ili hali idadi ya wabunge waliohitajika kupitisha muswada wanatakiwa wawe 233, ili mchakato huo uendelee.
Haya yanajiri huku msukumo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na Wakenya wa kawaida ukishika kasi, kutaka kufanyike kura ya maamuzi kwa lengo la kubadilisha katiba ya taifa hilo la Afrika Mashariki, katika kile kinachotajwa na wadau kama njia mojawapo ya kutatua matatizo ya kisiasa na kijamii yanayo ikabili nchi hiyo