Baada ya kitisho hicho cha Marekiani kutaka kujiondoa katika mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani INF, Rais Putin ameona ni busara kukutana na rais wa Marekani Donald Trump kwa mazungumzo mjini Paris.
Tangazo la kushtukiza la Trump kujiondoa katika mkataba huo limesababisha hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi wa mataifa ya Ulaya.
Hivi karibuni Putin Katika mkutano na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani John Bolton, mjini Moscow alisema yuko tayari kukutana na Trump hivi Karibuni. Wawili hao wanatarajiwa kuonana tarehe 11 Novemba pembezoni mwa sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia.
Bolton aliekuwa ziarani nchini Urusi amezungumzia mustakabali wa mkataba huo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov pamoja na mkuu wa baraza la usalama la Urusi Nikolai Patrushev.