Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 4:04 pm

NEWS: WAANDAMANAJI UFARANSA WAKATAA KUMTII RAIS MACRON

Waandamanaji walijitokeza jana siku ya Jumamosi jijini Paris na miji mingine nchini Ufaransa kuendelea kupinga nyongeza ya kodi kwa mafuta, licha ya wito wa rais Emmanuel Macron kuwataka wasijitokeze kuandamana.

Hata hivyo, idadi ya waandamanaji ilkuwa ndogo ikilinganishwa na Jumamosi zilizopita.

Waandaaji wanasema ni waandamanaji eldu 66 ndio waliojitokeza ikilinganishwa na 125,000 waliokuwepo Jumamosi iliyopita.

Mbali na suala la nyongeza ya kodi ya mafuta, waandamanaji hao sasa wanataka mabadiliko katika sekta ya elimu miongoni mwa mambo mengine.

Watu saba wamepoteza maisha katika maandamano hayo ya kila Jumamosi, huku mamia wakikamatwa.

Rais Emmanuel Macron amesema anawaelewa waandamanaji na kuwaomba waachane na maandamano hayo ya kila Jumamosi.