Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:38 am

NEWS : WAANDAMANAJI MAREKANI WPINGA UMILIKI HORELA WA SILAHA

Wamarekani waandamana wakitaka kubanwa umiliki wa silaha baada ya mauaji ya Texas

Wananchi wa Marekani wamefanya maandamano katika mji wa Washington kushinikiza kuangaliwa upya suala la umiliki na ruhusa ya kubeba silaha nchini humo, kufuatia mauaji ya makumi ya watu katika shambulizi la ufyatuaji risasi katika jimbo la Texas.

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba picha za baadhi ya wahanga wa mashambulizi ya silaha za moto na mabango yenye jumbe zinazosema: Kwa siku 1, vifo 91; Angalia Upya Sheria ya Kumiliki Bunduki, na kadhalika.

Jumapili iliyopita, watu wasiopungua 27 waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na askari wa zamani wa kikosi cha Jeshi la Anga la Marekani dhidi ya watu waliokuwa kanisani katika mji wa Sutherland Springs jimboni Texas.

Licha ya maelfu ya watu kuendelea kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika hujuma za ufyatuaji risasi nchini Marekani, lakini Rais Donald Trump wa nchi hiyo amekataa katakata kuzungumzia uwezekano wa kuangaliwa upya sheria ya raia kumiliki silaha nchini humo.

Shambulizi la Las Vegas la mwezi uliopita

Aidha mwezi uliopita wa Oktoba, watu wasiopungua 59 waliuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa baada ya mtu wa miaka 64 kwa jina la Stephen Paddock, kuwaminia risasi akiwa katika gorofa ya 32, karibu na eneo la Mandalay Bay katika mji wa anasa wa Las Vegas nchini Marekani.

Gazeti la Washington Times liliandika kupitia ripoti maalumu kuwa, kwa wastani watu 88 hupoteza maisha kila siku nchini Marekani katika matukio ya utumiaji silaha moto yakiwemo ya watu wanaojiua.