- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VYOMBO VYA HABARI 400 VYA MVAAA RAIS TRUMP
Zaidi ya magazeti 360 nchini Marekani yamechapisha HABARI zao leo Alhamisi kujibu kauli na Tuhuma za rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya vyombo vya habari ambavyo amekuwa akivishambulia kwa madai kuwa vinaandika habari za uwongo.
Kampeni hiyo ilioongozwa na gazeti moja la kila siku la mjini Boston inalenga pia kusisitiza juu ya umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari .
Gazeti hilo la The Boston Globe katika maoni yake ya mhariri limeandika kuwa nchini Marekani hivi sasa wana rais anaye amaini kuwa vyombo vya habari visivyounga mkono sera za serikali yake basi ni maadui wa watu na kuongeza kuwa huu ni mojawapo ya uwongo unaotolewa na rais Trump. Aidha gazeti hilo limesisitiza kuwa waandishi wa habari sio maadui.
Gazeti hilo la mjini Boston limeendelea kuandika kuwa kauli za rais Donald Trump dhidi ya vyombo vya habari pia zinawahamasisha marais wenye misimamo mikali kama vile Vladimir Putin wa Urusi na Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuwachukulia waandishi wa habari kama maadui.
Kampeni hii ya pamoja ya vyombo vya habari inakuja mnamo wakati rais Trump akiendelea kudai kuwa vyombo vikubwa vya habari vinavyochapisha na kutangaza habari zinazo mkosoa basi vinaandika habari ambazo yeye huziita habari za uwongo.
Wanaharakati wanaotetea uhuru wa vyombo vya habari wanadai kwamba hatua hii ya rais Trump inatishia uhuru wa vyombo vya habari katika kuandika ukweli pamoja na kuikosoa serikali pale vyombo hivyo vinapo kuwa na hisia za matumizi mabaya ya madaraka serikalini.
Aidha wanaharakati hao wanadai kuwa hatua hiyo ya Trump inakwenda kinyume na katiba ya Marekani inayosisitiza juu ya uhuru wa vyombo vya habari.
New York Times laandika kurasa saba
Gazeti la New York Times mojawapo ya magazeti yanayoshambuliwa mara kwa mara na Trump limeandika kurasa saba katika tahariri yake yenye kichwa cha habari kisemacho " A FREE PRESS NEEDS YOU": au Vyombo huru vya habari vinakuhitaji.
Aidha gazeti hilo limemueleza rais Trump kuwa ukweli asiopenda yeye kwake ndio anaita "habari za uwongo" hatua ambayo gazeti hilo limesema ni hatari kwa demokrasia nchini humo huku pia likisisitiza kuwa kuwaita waandishi wa habari kuwa ni maadui wa watu nayo ni hatari pia.
Kampeni hiyo ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari nchini Marekani imeungwa pia na vyombo vya habari vingine nchini kote huku pia wanaharakati wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari wakisema rais Trump ni kitisho dhidi ya ya vyombo vya habari.
Ken Paulson mhariri mkuu wa zamani wa gazeti la "USA Today" yeye kwa upande wake alisema hadhani iwapo vyombo vya habari vitaendelea kukaa kimya kwani vinapaswa kuchukua hatua pale vinaposhuhudia kiongozi mwenye nguvu kubwa duniani akijaribu kwenda kinyume na katiba.
Hata hivyo Paulson amehoji iwapo maoni hayo ya wahariri yatafanikiwa lengo lake na kufikisha ujumbe unaokusudiwa kwani wanaosoma maoni ya wahariri sio wale wanaowashambulia wakati wa mikutano ya rais.
Paulson amesema vyombo vya habari vinahitaji kampeni kubwa zaidi ya kuelezea kwa upana juu ya umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika jamii ikiwa ni pamoja na kufanyakazi ya ziada ya kufuta imani waliyo nayo baadhi ya wafuasi wa rais Trump wanaosema kuwa vyombo vya habari havitamuweza Trump.