- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VYAMA 10 VYA UPINZANI VYA FUNGUA KESI KUPINGA MUSWA WA VYAMA VYA SIASA
Dar es Salaam: Vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kwa minajiri ya kupinga muswada wa sheria wa vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria kamili.
Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.
Amesema muswada huo unalenga kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.
“Tunawaomba wanachama wetu wote kesho tufike kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi hii, wanademokrasia waone kwamba hatujakaa tunachukua hatua,” amesema Zitto
Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.