- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VODACOM WAFUNGUKA BAADA YA MKURUGEZI WAO KUNYINWA KIBALI
Dar es salaam: Kampuni ya Vodacom nchini Tanzania imethibitisha kuwa Mkurugenz wao Sylvia Mulinge ambaye ni raia wa Kenya aliyekuwa ameomba kibali cha kufanya kazi nchini amekwama kulingana na ombi lake kukataliwa na mamlaka za Nchi.
Mulinge alikuwa amepata Kandarasi ya wadhifa wa kuwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo ya huduma za simu nchini Tanzania na ombi lake limekataliwa na kamishna wa wafanyikazi nchini humo.
Kwa upande wao Vodacom inayofanya kazi chini ya kampuni ya Telecom imesema itaanza kumtafuta mtu mwingine atakayechukua wadhfa huo badala yake.
"Vodacom itasalia kuwajibika kumtafuta afisa ambaye sio tu atavutia imani ya wawekezaji bali pia kuwa na uwezo wa kuongoza kampuni hiyo", ilisema kampuni hiyo ya simu za mkononi.
Mwenyekiti wa Vodacom Tanzania , Ali Mufuruki alisema wana masikitiko makubwa kutokana na uamuzi uliotolewa lakini wataendelea kushirikiana na mamlaka ili kupata mtu mwingine anayefaa kuwa katika nafasi hiyo.
Taarifa hiyo haikuelezea sababu ya kukataliwa kwa raia huyo wa kenya , lakini vyombo vya habari vimeripoti kwamba serikali ya tanzania inaamini kuna Watazania wengi walio na uzoefu wanaoweza kuchukua wadhfa huo.
Sylvia Mulinge ambaye alitakiwa kuanza kazi yake nchini Tanzania tangu mwezi Juni mwaka huu alishindwa kuanza kazi hiyo baada ya kuchelewa kwa kibali chake.