Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:03 am

NEWS: VIJANA 7 WALIOKANYAGA PESA ZA NOTI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Dar es salaam: Vijana 7 wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kizutu leo Oct. 2 wakikabiliwa na kesi ya kuharibu noti za banki kuu ya Tanzania za Tsh 70,000 kwa kuzikanyaga kanyaga.

Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Vicent Kaduma (24), Rogers Swale (23 ), Doreen Mwenisongole (22) ni mwanafunzi, Kelvin Mngeyekwa 23, Eia Chengula 24 mfanyabiashara, Said Sadiq 21 na Ramadhan Seleman 23.

Akisoma hati ya mashtaka, chini ya kifungu cha 332 A cha kanuni ya adhabu, mbele ya Hakimu Mkazi Wanjah Hamza wakili Kombakono amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa moja la kuharibu noti za BoT.

Imedaiwa, Septemba 16 mwaka 2018 washtakiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam, pasipokuwa na mamlaka waliharibu noti za Sh.70,000 ambazo noti moja ilikuwa na thamani ya Sh. 10,000.Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya mahakama kupatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 waaminifu waliosaini bondi ya Shilingi Milioni 2 kila mmoja. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 11 mwaka 2018.