- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIGOGO WENGINE WA ACACIA WANASWA NA TAKUKURU
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika na Mshauri wa serekali ndani ya Kampuni hiyo Alex Lugendo.
Akizungumza jana, na Kampuni ya MCL Digital naibu mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema wanawashikilia wawili hao tangu juzi na leo wanaweza kufikisha mahakamani kwa hatua zaidi.
“Tumewakamata kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi katika tasnia ya madini,” alisema Mbungo.
“Lakini hawa wakiwa viongozi waandamizi walishindwa kusimamia nchi ipate mapato kama ilivyotakiwa.”
Naibu mkurugenzi huyo alisema wamefanya mahojiano na watuhumiwa hao kwa kipindi kirefu.
“Baada ya kukamilisha mahojiano tangu tulipowakamata jana (juzi), leo (jana) tuliwapeleka mahakamani lakini kutokana na sababu zilizojitokeza walishindwa kupandishwa kizimbani lakini kesho (leo) natarajia itawezekana,” alisema
Mwanyika aliyejiunga na Acacia mwaka 2001 akiwa ameitumikia kampuni hiyo kwa nafasi mbalimbali kwa miaka 17, alitangazwa kujiuzulu Agosti 24 kwa barua ya ofisa mtendaji mkuu wa Acacia, Peter Galeta kwenda kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.