- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIGOGO KESI YA ALMASI WALALAMIKA KUFA NJAA NA FAMILIA ZAO
Dar es Salaam: Hakimu Mkazi Mkuu Respicius Mwijage, amewaagiza Wakili wa Serikali, Simon Wankyo na wakili wa washtakiwa, Nehemia Nkoko ombi la maafisa wa serekali Mkurugenzi wa Tathmini, Archard Kalugendo (49) na mthamini wa madini ya almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu (50)wanaoshtakiwa kwenye sakata la kutoroshwa kwa Almasi , wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasaidie waweze kupata kadi zao za benki walizonyang'anywa walipokamatwa.
Maafisa hao wametoa ombi hilo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage shauri hilo lilipotajwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu Jiji Dar es salaam.
Washtakiwa wanaomba kurejeshewa kadi hizo wakisema wana familia na mishahara yao inapitia benki.
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Mwijage amewaagiza Wakili wa Serikali, Simon Wankyo na wakili wa washtakiwa, Nehemia Nkoko walifanyie kazi ili familia za washtakiwa zisije kufa kwa njaa.
Amesema kuna maeneo walikuwa wakiyafanyia kazi ambayo yameshakamilika na wanapanga kupeleka jalada kwa DPP.
Wankyo amesema tarehe ijayo wataeleza hatua waliyofikia.Kwa upande wake, wakili Nkoko amesema taarifa iliyotolewa na upande wa mashtaka ni hatua nzuri. Ameomba juhudi zifanyike katika upangaji wa jalada.
Hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 9,2017. Ameagiza upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi ili kesi iendelee.
Washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kusababisha hasara ya Dola 1.118 milioni za Marekani sawa na Sh2.486 bilioni.
Kalugendo ambaye ni mkazi wa Kinyerezi na Rweyemamu wa Mwananyamala ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.
Wanadaiwa kati ya Agosti 25 na 31,2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiliwa na Wizara ya