- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIFAA VYA TUME YA UCHAGUZI CONGO VYATEKETEA KWA MOTO
#BreakingNews: Ghala kubwa lililokuwa limehifadhi vifaa vya tume ya uchaguzi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, limeteketea kwa moto, vyanzo rasmi kadhaa vimelithibitishia likiwemo shirika la habari la AFP, mjini Kinshasa.
Moto huo uliozuka katika ghala hilo usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii umesababisha hasara kubwa. Vifaa viliokuwa katkaghala hilo karibu vyote vimetekea kwa moto.
Tukio hilo linatokea ikiwa zimesalia siku kumi kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23.
"Moto ulizuka karibu saa nane usiku saa za Kinshasa (sawa na saa saba saa za Afrika ya Kati) katika moja ya ghala kuu ambapo kulikuwa kumehifadhiwa vifaa vya uchaguzi katika mji wa Kinshasa," amesema mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), Korneille Nangaa.
Wingu kubwa la moshi mweusi lilikuwa bado linaonekana saa mapema alfajiri, kwa mujibu wa televisheni ya shirika la habari la AFP.
Vifaa vya uchaguzi vilivyokuwa vimehifadhiwa katika ghala hilo ni pamoja na "mashine za kupigia kura" ambazo upinzani unapinga kutumiwa katika uchaguzi wa Desemba 23, ukidai kuwa zimepangwa kutumiwa kwa kuiba kura.