- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: VIBARAKA WA CCM WASALITI KIAMA CHAO KIMEKARIBIA.
DODOMA: Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Kheri James amesema wale wanaccm vibaraka wenye lengo la kuharibu heshima na kubomoa misingi ya chama hicho muda wao umekwisha.
Ameyasema hayo desemba 13 wakati akipokelewa na wanauvccm katika sherehe hizo zilizofanyika katika jengo la Ccm mjini Dodoma.
James amesema haiwezekani chama kinapanga kanuni na utaratibu za kuleta maendeleo katika taifa lakini baadhi ya watu wanakuwa wasaliti.
"Lazima kuheshimu misingi na sheria ya chama haiwezekani sisi watu wazima tunakaa tunapanga mikakati mtu anatokea tu anaharibu," amesema James.
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na wilaya kuanza kufanya ukaguzi/uhakiki wa Rasilimali za Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) katika maeneo yao.
Mbali na hayo amewahimiza Umoja na mshikamano kwa Vijana wote ndani ya jumuiya hiyo ili kufanya kazi kwa umoja na kutimiza malengo kwa wakati.
“ Vijana tunapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Rushwa na sio kuwaachia Viongozi pekee ,tunapaswa kutambua kuwa rushwa ni adui mkubwa wa haki na hivyo ni jukumu letu kuwa na umoja na mshikamano kukumea,”amesema.
Hata hivyo James amewafahamisha kuwa umoja wa vijana utafanya kila linalowezekana kulinda uhai na hadhi ya Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuwaonya waumini wa makundi ya uchochezi na kuwagawanya watu kuwa katika uongozi wake hatavumilia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni katiba na taratibu za jumuiya na chama.
Vile vile amefahamisha kuwa awamu ya kwanza ni kupokea wanachma wapya na hatua inayofuata ni kukabidhiwa mpaka majengo yao kwa vile watakosa wafuasi wa kuyatumia.
Katika mapokezi ya Mwenyekiti na Makamu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) walipokea wanachama wapya 200 kutoka vyama mbalimbali vya Siasa nchini ikiwemo Chama cha demokrasia na maendeleo.