Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:25 pm

NEWS: UWASHERATI WAITIKISA SHULE YA SEKONDALI MAKOLE.

DODOMA: uwasherati umeonekana nikikwazo kikubwa katika shule ya sekondari ya makole ambapo jumla ya wanafunzi 6 Wa kidato cha nne waligundulika kuwa na ujauzito kwa mwaka huo.

Akisoma risala wakati wa maafa ya kidato cha nne yalifanyika leo mjini hapa Wanafunzi mhitimu Wa shule hiyo Jacklin Muzilai amesema wapo baadhi wa wanafunzi waojihusisha na mahusiano na kupelekea kukatisha ndoto zao.

"Kuna mwanafunzi wenzetu sita kwa mwaka huu wamekatisha masomo yao kwa kubeba mimba wakiwa shuleni", amesema.

Akifafanua zaidi amesema miongoni mwa changamoto zingine ni pamoja na kosefu wa matundu ya vyoo,utoro,uhaba Wa maabara na ukosefu wa miundombinu.

‘’Ukosefu wa matundu ya vyoo kwa wavulana na wasichana ambapo matundu ya vyoo ni manne na idadi ya wavulana wa shuleni hapa wapo 306’’, amesema.

Amesema ili kuboresha taaluma ya shule ni muhimu changamoto hizo zikatatuliwa kwa wakati.

Naye mwalimu mkuu Wa shule hiyo Amani Mfaume amesema shule yao inakabiliwa na changamoto Wa ukosefu Wa nyumbani za walimu pamoja na uhaba Wa vyoo .

" Kuna baadhi ya vyoo vinavyotumiwa na walimu haviendani na hadhi yao" alisema.

Kwa upande wake Mchungaji Wa kanisa la Agape Revival Temple Ipagala (T.A.G) ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Alex Makunguru Amewataka wazazi kushirikiana na walimu ili kuleta ufaulu mzuri kwa mwanafunzi.

"Ili makole iende mbali unahitajika ushirikiano kati ya wazazi na walimu", amesema.

Wazazi kukaa Karibu na watoto wao ili kuwaelimisha juu ya athari mbalimbali zilizopo kwenye jamii ikiwemo ya kukaa vijiweni pamoja na kuvaa mavazi yasivyo na maadili.

" Sisi kama wazazi inatufaa kuwasongelee tuwalee watoto wetu ili kujenga kizazi chenye nidhamu",amesema.

Pia amewasisitiza mwanafunzi hao kuvaa mavazi yenye hekima ili kuleta tabia njema kwa jamii.

" Ili kuonekana mzazi bora unahakikisha unamrithisha Elimu mtoto wako",amesema.

Mbali na hayo alimpongeza Waziri Wa Tamisemi Selemani Jafo kwa mchango Wa nunuzi Wa madawati.

Katika maafa hayo jumla ya wanafunzi 83 wamehitimu Elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.