Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:41 pm

NEWS: UTUMIAJI WA VYETI 'FEKI' NI KUSHUKA KWA MAADILI KATIKA TAIFA.

DODOMA: Imeelezwa kuwa utengenezaji na utumiaji wa vyeti feki na udanganyifu katika matumizi ya vyeti vya elimu ili kusoma na kupata kazi kwa njia isiyo halali imeonekana ni miongoni mwasababu inayochangia kushuka kwa maadili katika taifa letu.

Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha st John’s Prof Emanuel Mbennah wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya chuo hicho yaliyofanyika mjini hapa.

Aidha Prof Mbennah ameongeza kuwa miongoni mwa sababu nyingine zinazochangia kushuka kwa maadili katika taifa letu ni pamoja na kuwepo kwa roho ya ubinafsi,suala la watumishi hewa katika sekta mbalimbali za utumishi, na watumishi wasio waamini jambo ambalo linasababisha kushindwa kusimamia kazi katika maeneo yao.

Pia amesema wanafunzi kutoa rushwa za ngono na fedha ili kupasishwa mitihani na kuendelea na elimu wasiyostahili , jambo ambalo linadhaoofisha ubora wa elimu katika taifa letu.

Mbali na hayo amesema lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho ni kupata viongozi bora na wataalamu katika taifa watakaokuwa na hofu ya mungu ambayo itasaidia kuinua uadilifu katika maisha na utumishi wao.

Hata hivyo amesema chuo hicho kililenga kujenga wahitimu waadilifu , ili kusaidia kuwa na msukumo wa kutumika badala ya kutafuta kutumikiwa na watu wengine

Ndoto za kuanzishwa Kwa Chuo hicho zilianza 1999 ambapo maaskofu walikaa na kujadili na rais wa awamu ya nne Dk Jakaya mrisho kikwete nakukubaliana kuanzishwa rasmi 2007.