- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: URUSI YATISHIA KUUNDA MAKOMBORA YALIYOPIGWA MARUFUKU DUNIANI
Moscow: Vyomba vya habari nchini Urusi vimemnukuu kiongozi wa juu wa taifa hilo Rais Vladimir Putin akisema kuwa Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi kama taifa la Marekani litajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo.
Putin amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.
Katika tamko hilo lililoangaziwa kwenye televisheni, kiongozi huyo alisema mataifa mengi yanaunda silaha zilizopigwa marufuku katika mkataba wa INF
"Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaonelea ni lazima wao pia wawe na silaha ," alisema.
"Jibu letu ni nini? Bila shaka - sisi pia tutafuata mkondo huo."
Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).
Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri.