- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: URUSI YASHUTUMIWA KUSAFIRISHA MAFUTA KOREA KASKAZINI KWA SIRI
Moscow: Nchi ya Urusi imeshukutumiwa baada ya kuonekana ikisafirisha mafuta kwenda Serekali ya Pyongyang nchini korea kaskazini, kwa mujibu wa Maafisa wawili wa usalama barani Ulaya wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba malori mawili ya mafuta kutoka Urusi yaliwasilisha mafuta huko Korea Kazkazini hivyo kukiuka azimio la umoja wa mataifa la kuzidisha vikwazo zaidi dhidi ya utawala huo wa Pyongyang ili kujaribu kukomesha mradi wake wa kutengeneza silaha za kinuklia.
Maafisa hao Wanasema kuwa malori hayo yaliyosafirishwa kwa meli yalionekana katika picha za Satellite zilizo karibu na bandari za Urusi upande wa pwani ya Pacific na kuthibitishwa kwa duru za kiintellijensia .
Hata hivyo mmoja wa maafisa hao ameongeza kusema kuwa bado hamna ushahidi wowote kwamba serkali ya Urusi imehusika na usafirishwaji wa shehena hiyo.
Meli husika ambayo iko chini ya leseni ya Hong Kong ilikamatwa na maafisa wa Korea Kusini lakini mwenye meli hiyo amekana kuhusika na swala hilo.