- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UPINZANI ZIMBABWE NA CHAMA TAWALA WOTE WAJITANGAZIA USHINDI
Harare: Rais wa sasa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na kiongozi mkuu wa upinzani Nelson Chamisa, wote wanadai kuwa wanaelekea kupata ushindi mkubwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu.
Mnangangwa amesema, chama chake cha ZANU-PF kinapata matokeo mazuri huku Chamisa akisema chama chake cha MDC kinaelekea kupata ushindi mkubwa.
Kauli hii inaonesha kuwa, matokeo ya mwisho, yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi kufikia mwisho wa wiki hii, yatazua mzozo kati ya wanasiasa hao wawili kuhusu mshindi wa kweli.
Kuelekea katika Uchaguzi huo wa kihistoria ulioshuhudia zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura wakijitokeza, upinzani ulidai kulikuwa na njama za Tume ya Uchaguzi kumsaidia Mnangagwa kushinda uchaguzi huo.
“Taarifa tunazozipata kutoka kwa wawakilishi wetu, zinaonesha kuwa tunapata ushindi, lakini tunasubiri matokeo kwa mujibu wa Katiba,” amesema Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Naye Chamisa mwenye umri wa miaka 40, amenukuliwa akisema wako tayari kuunda serikali mpya.
“Tunaelekea kupata ushindi mkubwa sana, tumefanya vizuri na tuko tayari kuunda serikali mpya,” amesema Chamisa kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Huu umekuwa ni Uchaguzi wa kwanza, kufanyika bila ya kuwepo kwa rais wa zamani Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani mwaka 2017, baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 1980.
Waangalizi wa kimataifa wamesema kwa mara ya kwanza, wapiga kura walijitokeza na kupiga kura bila vitisho au vurugu.
Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa yeyote atakayeshinda, anatarajiwa kuleta mabadiliko nchini humo.