- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UPINZANI UKINGONI WANACHAMA 411 WATUA CCM.
DODOMA: Chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma mjini kimezindua kampeni ya Kuongeza idadi ya wanachama ya Kata kwa kata, huku Jumla ya wanachama 411 kutoka vyama vya Upinzani na wafanyabiashara wadogo (wamachinga) wakikabidhiwa kadi ya uwanachama wa CCM.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo mjini hapa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Dodoma mjini Daniel Mwinje huku Akisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuongeza wanachama na kuuwa upinzani katika mkoa hupo.
Pamoja na hayo amesema Dodoma bila Upinzani inawezekana kama wanachama wa CCM pamoja na viongozi watafanyakazi kwa kushirikiana nakwa juhudi kubwa.
Mbali na hayoMinje amempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDk John Magufuli katika juhudi kubwa za kuleta maendeleo katika Taifa ikiwemo kupiga vita rushwa, kusimamiavizuriukusanyaji wa kodi .
Aidha ameendelea kumpongeza rais kwa jitihada kubwa ya kusimamia nidhamu kwa watumishi wa Umma pamoja na kuendelea kujenga viwanda nchini.
Ameongeza kuwa juhudi za serikali kuhamia Dodoma zitaufanya mkoa kuwa na miundombinu mizuri ikiwemo kuboreshaujenzi wa shule na kuleta fursa kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Hata hivyo amempongeza rais kwa kuivunja CDA maana CDA ilionekana ni changamoto kubwa katika mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake katibu wa siasa na uenezi mkoa wa DodomaHenry Msunga amesema kuwa mwana _ CCM ni kiungo kati ya chama cha serikali hivyo kama wanachama wanapaswa kujivunia .
Amesema CCM ni chama salama kinachowajali wananchi kitahakikisha kata hiyo inarudi mikono mwa chama hicho.
Uzinduzi wa Kampeni ya kuongeza idadi ya wanachama wapya kutoka kata kwa kata umeanzia katika kata ya Madukani ambapo zamani kata hiyo ilikuwa na wananchama 524 baada ya kujiunga wanachama wapya 411 mpaka sasa kata hiyo inajumla ya wanachama 935.