Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:49 pm

NEWS: UPINZANI NCHINI KENYA WACHEZEA KICHAPO CHA POLISI LEO

Nairobi: Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA umelaani vikali matumizi makubwa ya nguvu wanayo tumia Polisi nchini kenya dhidi ya wafuasi wake walioandamana hivi leo kwenye miji mbalimbali nchini humo ambapo polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kwamujibu wa wakili wa NASA James Orengo amesema kuwa muungano wao unasikitishwa na namna ambavyo polisi walishindwa kuheshimu amri ya mahakama na kuwatawanya wafuasi wake waliokuwa wakiandamana kwa amani.

Orengo amesema licha ya hapo jana kukutana na mabalozi wa Marekani na Uingereza na kuwahakikishia kuwa polisi hawatazuia maandamano yao, wameshangazwa namna ambavyo polisi walitumia nguvu kuwafurusha wafuasi wao.

Orengo amewakashifu vikali mabalozi wa nchi hizo akisema waliwadanganya kwa kuwapa hakikisho kuwa Serikali iliwahakikishia kuwa haitaingilia maandamano yao lakini hali ilikuwa kinyume.

NASA inasisitiza kuwa itaendelea mbele na maandamano yao hapo kesho licha ya kuwa wanafahamu fika polisi wataendelea kutumia mabavu kuzuia nguvu ya uma dhidi ya tume ya uchaguzi IEBC.

Katika hatua nyingine kinara wa NASA Raila Odinga ambaye amejiondoa kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa juma hili, amekana kuwa aliwaamrisha wafuasi wake kuandamana siku ya kupiga kura na badala yake anasema alichowaambia ni kususia uchaguzi huo.