- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UPINZANI NCHINI CONGO WAGOMEA UCHAGUZI UJAO
Muungano wa upinzania usio rasmi nchini DRC Congo wanakataa kuunga mkono uchaguzi wa Desemba 23 ambao wanadai kuwa "hautokua wa haki" na "utasababisha machafuko nchini".
hapa ni Wagombea wa upinzani waliothibitishwa na wale waliotengwa katika uchaguzi wote kwa pamoja wamekubaliana
"tume ya uchaguzi CENI na serikali watakua wamehusika na uhasama na machafuko kutokana na kuundaa kwao uchaguzi ambao utakua umegubikwa na ujanja fulani," wamesema katika taarifa yao ya pamoja.
Wakati wa mkutano huko Brussel nchini Ubelgji Jumatano wiki hii, wanasiasa hao wakuu wa upinzani walitoa baadhi ya masharti na kutoa wioto kwa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) kuachana na mpango wa kutumia mashine ya kupigia kura katika uchaguzi huo.
Kama CENI haitosikia malalamiko yetu kuhusu mashine hiyo ya kupigia kura "raia watachukua maamuzi, kwa sababu CENI haiko juu ya sheria wala haina uzito wowote mbele ya wananchi. Uchaguzi unaandaliwa kulingana na makubaliano kati ya pande husika. Hakuna upande ambao unapaswa kuweka sheria kwa wengine, "alisema Vital Kamerhe, mmoja kati ya wagombea urais waliokubaliwa kuwania uchaguzi , baada ya kutia saini kwenye taarifa ya pamoja.
Wagombea wawili wa upinzani waliokubaliwa na Mahkama ya Katiba kuwania katika uchaguzi wa Desemba 23, Felix Tshisekdi na Vital Kamerhe, na wengine wawili waliotengwa, Jean-Pierre
Bemba na Adolphe Muzito pamoja na Moise Katumbi,ambaye alizuiwa kurejea nchini kuwasilisha kuwasilisha fomu yake kuwania katika uchaguzi huo na Mbusa Byamwisi, walitia saini kwenye taarifa hiyo ya pamoja.
Wameomba wagombea waliotengwa kukubaliwa kuwania katika uchaguzi ujao, huku wakitoa wito kwa CENI kuachana mpango wa kutumia mashine ya kupigia kura.
Hata hivyo, wameahidi "kukubaliana kuteua mgombea mmoja ambaye atapambana katika uchaguzi huo na mgombea wa chama tawala ili kupata kura nyingi kwa minajili ya kushinda uchaguzi."