Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 2:35 pm

NEWS: UNAAMBIWA KUWA JIJI LA DAR LINASHIKA NAFASI YA PILI KWA UTAJIRI

Ripoti ya New World Wealth pamoja na benki ya AfrAsia nchini Mauritius, inasema kuwa utajiri wa jiji la Dar es Salaam unathamani ya $25 bn hii ni kwa mwaka 2017 na kwa utajiri huo linashika nafasi ya 2 nyuma ya jiji la Nairobi kwa Afrika mashariki na linakuwa jiji la 12 barani Afrika wakati jiji la Nairobi linakuwa la 6.

Utajiri huo umetokana miongoni mwa mengine na viwango vya utajiri wa watu binafsi (HNWIs) na pia katika mapato yanayoingia katika sekta ya starehe barani Afrika kama hoteli na vivutio vingine.

Kwa jumla ripoti hiyo inakadiria kuwa sekta hiyo ya starehe barani Afrika imechangia takriban $ bilioni 6.0 za mapato mnamo 2017.

Kwa kuangazia kiwango cha ongezeko la utajiri, mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, isipokuwa Burundi, ni miongoni mwa nchi ambazo zimeimarika pakubwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Mauritius inaongoza kwa ukuaji wa asilimia 192 ikifuatwa na Ethiopia iliyokuwa kwa asilimia 190.

Baada ya hapo, mataifa ya Afrika Mashariki yanafuata yakiongozwa na Rwanda (74%), Kenya (73%), Tanzania (66%), na Uganda (53%).


MjiUtajiri kwa Mabilioni ya Dola
1. Johannesburg276
2. Cape Town155
3. Cairo140
4. Lagos108
5. Durban55
6. Nairobi54
7. Luanda49
8. Pretoria48
9. Casablanca42
10. Accra38
11. Abidjan27
12. Dar Es Salaam25
13. Alexandria25
14. Kampala16
15. Windhoek13
16. Abuja13
17. Addis Ababa13
18. Marrakesh11
19. Tangier11
20. Lusaka10
21. Maputo10
22. Gaborone9
23. Mombasa