- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : UMOJA WA MATAIFA WALAANI ONGEZEKO LA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI DRC
Umoja wa Mataifa walaani ongezeko la ukiukaji wa haki za binadamu DRC
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limelaani ongezeko la vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za kukomesha vitendo hivyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch ni kuwa, vitendo vya ukiukaji haki za binadamu vimeongezeka kwa asilimia 63 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ripoti hiyo ya Human Rights Watch inaeleza kuwa, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, visa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo vimeongezeka kwa asilimia 60.
Aidha ripoti zaidi zinasema kuwa, wanaharakati na wafanyakazi wa asasi za kiraia ndio ambao wamekuuwa wakilengwa zaidi katika matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi hiyo. Polisi, jeshi na vikosi vya usalama vimekuwa vikitajwa kuwa, vinahusika na matukio mengi ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.
Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Jose Maria Aranaz, Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo alitangaza kuwa, wanajeshi 104 na polisi 20 wa nchi hiyo waliopatikana na hatia ya kukiuka haki za binadamu wameshtakiwa na kuhukumiwa adhabu mbalimbali katika kipindi cha miezi sita ya awali ya mwaka huu.
Serikali ya Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo imekuwa ikionyeshewa kidole cha lawama hasa kutokana na kufanya njama za kuendelea kubakia madarakani na wakati huo huo kuwakandamiza wapinzani.