- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : UMOJA WA MATAIFA WAKIRI HALI YA UKANDA WA GAZA NI YA MGOGORO
Mratibu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mashariki ya Kati, usiku wa kuamkia leo Alkhamisi amesema kuwa, hali katika eneo la Ghaza huko Palestina ni ya mgogoro.
Nikolay Mladenov amesema hayo katika kikao cha kila mwezi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matukio ya Mashariki ya Kati na kuutaka utawala wa Kizayuni uache kutumia nguvu na kufanya mauaji ya kiholela dhidi ya Wapalestina wanaofanya maandamano ya amani katika Ukanda wa Ghaza.
Hivi karibuni pia mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mashariki ya Kati alionesha kukasirishwa sana na jinai za utawala wa Kizayuni za kuua watoto wadogo katika maandamano makubwa ya 'Haki ya Kurejea' na alisema kuwa, kitendo cha wanajeshi wa Israel cha kuwadungua kwa risasi watoto wadogo wa Kipalestina ni aibu.
Maandamano ya amani ya 'Haki ya Kurejesa' yalianza tarehe 30 Machi mwaka huu kwa mnasaba wa 'Siku ya Ardhi' na kwa ajili ya kupigania haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea katika ardhi zao za jadi.
Hata hivyo wanajeshi makatili wa Israel wamekuwa wakifanya mauaji ya umati dhidi ya wananchi hao wa Palestina kiasi kwamba hadi hivi sasa zaidi ya Wapalestina 112 wameshauwa shahidi wa kupigwa risasi na wanajeshi hao madhalimu na karibu 13,000 wengine wameshajeruhiwa.
Duru za hospitali za Palestina zimetangaza kuwa, watoto wadogo 13 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa shahidi hadi hivi sasa kwa kupigwa risasi za wanajeshi makatili wa Israel.