- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : UMOJA WA MATAIFA WAANZA KUFANYA UPEKUZI NCHINI KONGO DRC
Umoja wa Mataifa wataka kukamatwa watu waliouwa wataalamu wake Congo DR
Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoa ushirikiano katika jitihada za kuweka wazi kadhia ya mauaji ya wataalamu wake wawili nchini humo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchunguzi kuhusu mauaji ya Michael Sharp na Zaida Catalan katika mkoa wa Kasai mwezi mapema mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amemteua mwendesha mashtaka Mcanada, Robert Petit na wataalamu wengine kadhaa kwa ajili ya kuisaidia mahakama ya kijeshi ya Congo kuweka wazi kadhia ya mauaji ya wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limeitaka serikali ya Kinshasa kushirikiana na wataalamu hao kwa ajili ya kutekeleza uadilifu na kuwatia nguvuni watu waliotenda jinai hiyo.
Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walikuwa nchini Congo kwa shabaha ya kuchunguza kesi za ubakaji na ukatili wa kingono uliodaiwa kufanywa na waasi nchini humo.