- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UMOJA WA MATAIFA KUIWEKEA VIKWAZO SAUDI ARABIA
New York: Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mashirika ya kutetea haki za binadamu, wanaharakati mbalimbali kutoka pembe za Dunia na vyama vya waandishi wa habari vimetaka waliohusika na mauaji ya mwandishi habari wa Habari wa Gazeti la Washington Post Jamal Khashoggi nchini Uturuki waadhibiwe kivikali.
Guterres amesema amepata wasiwasi mkubwa baada ya Saudi Arabia kukiri kuwa Khashoggi alifikwa na umauti kwenye ubalozi wake mdogo. katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ameongeza kusema kuwa kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusiana na kadhia hiyo ili waliohusika wachukuliwe hatua. Uturuki imeelezea kutokufurahishwa nanhatua ya Saudi Arabia ya kuchelewa kukiri kwamba imehusika na mauaji ya Khashoggi na kukitaja kitendo hicho kuwa cha kufedhehesha.
Shirika la Amnesty International limesema maelezo ya Saudi Arabia kuhusu mauaji ya Khashoggi yanaonekana kufunika mauaji ya kinyama,na taarifa nyingine mbaya zinazodhihirisha kwamba Saudi Arabia inakiuka haki za binadamu. Shirika hilo la Amnesty International limeitaka nchi hiyo kuutoa mwili wa mwandishi huyo wa habari ili ufanyiwe uchuguzi kubainisha chanzo cha kifo chake.
Taarifa ya vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imeongeza kusema kuwa mshauri wa mahakama ya Saudi Arabia, Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi