Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 6:47 pm

NEWS: UMMY AHIDI KUFUNGA MASHINE MPYA YA X-RAY MTWARA

Mtwara: Waziri wa Afya, Jinsia na Watoto na walemavu Ummy Mwalimu amesema hali ya upatikanaji wa dawa muhimu katika hospitali ya Rufaa Mtwara ni asilimia 94%

Huku akisema kuwa Huduma za Maabara zinapatikana vizuri katika hospitali hiyo.

Kauli hiyo ya Ummy ameitoa leo Siku Jumanne Dec 4, 2018 baada ya kutembelea hospitalini hapo.

Hata hivyo Ummy amesema ipo changamoto ya mashine ya X-Ray, ambayo imeharibika takribani siku 4 sasa.

"Tayari matengenezo yanaendelea. Pia, tutaleta mashine mpya ya X-Ray before end of Feb 19" amesema Ummy.