- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UMMY AFUNGUKA KUHUSU MFUKO WA NHIF.
DODOMA: Ili kufanya mfuko wa NHIF kuwa endelevu ,mfuko huo huwekeza katika fedha za ziada katika vitega uchumi mbalimbali vya muda mfupi na mrefu vyenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa ujumla wake.
Akijibu swali la mbunge wa Tumbe Rashid Ally aliyetaka kujua kuwa je , ni utaratibu gani wa kisheria uanafanyika ili kuhakikisha fedha za wanachama zinalindwa.
Waziri wa afya, maendeleo jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema uwekezaji wa unaofanywa na NHIF ni jukumu mojawapo la kisheria linalotekelezwa chini ya kisheria linalotekelezwa chini ya sheria ya mfuko wa bima ya afya ya mwaka 1999 ambao pia unasimamiwa na sera ya NHIF ya uwekezaji pamoja na miongozo ya uwekezaji kama ilivyotolewa na mamlaka ya usiaminzi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) ikishirikiana na beki ya Tanzania (BOT).
Mbali na hayo amesema kazi mojawapo ya msingi ya mamlaka ya usimaminzi wa sekta ya hifadhi ya jamii ikishirikiana na benki kuu ya Tanzania ni kutetea na kulinda maslahi ya wanachama kwa kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya jamii inaelekeza uwekezaji wake katika vyanzo vya uwekezaji vilivyo salamana vyenye tija kwa wanachama na taifa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Tathiminiya 4 ya uhai wa mfuko iliyofanywa mwaka 2013 inaonyesha uwezo wa mfuko kifedha na uendelevu wake ni hadi kufikia mwaka 2040.