- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UKOSEFU WA MAJI WAWATESA WANANCHI WA NG'ONG'ONA DOM.
DODOMA: Wananchi wa kata ya Ng,ong,ona manispaa ya Dodoma wamelalamikia suala la ukosefu wa maji safi na salama kwa kipindi cha muda mrefu .
Wakizunguza kwa nyakati tofauti moja ya wananchi hao Juma Yusuph walisema wanashangazwa kuona ni muda mrefu sasa tangia nchi kupata uhuru lakini suala ya maji linaonekana ni kikwanzo kikubwa katika kata hiyo.
‘’Mimi tokea nizaliwe yaani nimezaliwa nimelikuta hili janga lipo mi nafikiri hili janga tokea nchi ipate huru halijawahi kutatuliwa,’’alisema Yusuph
‘’Takribani mita 300 kutoka katika maeneo yetu hadi kilipo chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) chenye miundombinu yote,’’alisema.
Licha ya tatizo hilokuwepo wanalazimika kununua maji kwenye mabonza kwa gharama ya Sh 300 kwa ndoo moja jambo linalowaghalimu kiuchumi.
‘’ Hili tatizo limekuwepo kwa muda mrefu tokea enzi za mababu walivyokuwepo mpaka leo wajukuu tumezaliwa tumelikuta lakini hali bado ikopalepale mtu unanunua ndoo moja Sh 300 je kwenye familia unatumia ndoa ngapi,’’alisema.
kwa upande wake diwani wa kata hiyo Philipo Namga alisema licha ya jitihada kubwa wananazozifanya bado tatizo hilo limeendelea.
Mbali na hayo aliongeza kuwa kulikuwepo na mradi wa maji ulianza mnamo mwaka 2012 ambapo wahusika wakuu katika mradi huo ni manispaa ya Dodoma lakini mpaka sasa ni miaka sita mradi huo haujaweza kufanyika.
‘’Kwa kweli suala la maji katika mtaa huu wa Ng’ong’ona bado limekuwa sugu sana limekuwa la muda murefu sana kama takribani miaka 40 watu hawapati maji safi,’’alisema Namga.
Aidha alisema jitihada zingine ni kushirikiana na mamlaka ya maji safi na usalama wa mazingira (DUWASA)lakinitatizo lipo bado halijaweza kupatiwa ufumbuzi.
Naye mhandisi wa manispaa ya Dodoma Walter Kirita alisema kuwa tayari mradi huo wa maji wamekwisha ukabidhi Duwasa na utaanza kushugulikiwa kuanzia mwezi desemba na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuwa na subra kwani kuanzia mwezi january mwakani maji yataanza kupatikana.