- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: UKOSEFU WA AJIRA VYUO VYA SERIKALI ZA MITAA BADO KITENDAWILI KIGUMU.
DODOMA: Ukosefu Wa ajira nchini imeonekana ni moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wanaohitimu vyuo mbalimbali vya serikali za mitaa ikiwemo chuo cha Hombolo(logiso) mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na rais Wa wanafunzi Ibrahim Rashid Wakati akisoma risala ya maafali ya Tisa ya chuo hicho yaliyofanyika mjini hapa.
Amesema miongoni mwa changamoto nyingine ni ukosefu Wa mikopo kwa wanafunzi, upungufu Wa miundombinu ikiwemo Maji na barabara na uhaba Wa wafanyakazi katika chuo hicho.
Mbali na hayo ameiomba serikali kuanzisha mafunzo ya shahada ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kujiendeleza chuoni hapo na kuiomba serikali iwasaidie katika kutatua changamoto zilizopo ili kuboresha Elimu na kuleta utawala bora ndani ya taifa letu.
Naye Mkuu wa chuo hicho Dr Mpamila Madala ameongeza kuwa kama chuo kimeandaa mafunzo mbalimbali Ikiwemo kuandaa semina enezi ili kuwawezesha kuandaa andiko, chuo kimeweza kuandaa tafiti nane pamoja na kuwasongezea Maji safi na salama katika kutatua changamoto zinazowakabiri.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye ni Waziri Wa Tamisemi Selemani Jafo amesema kama serikali itafanya jitihada ziwezekano ili kutatua changamoto ya ukosefu Wa miundombinu.
Aidha amewataka wahitimu hao kutofanyakazi kwa mazoea pindi wawapo katika nyanja mbalimbali za kiutendaji.
Hata hivyo Jafo ameongeza kwa kuwataka wanafunzi hao kufanyakazi kwa weledi na kwa uwamini ili kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya Viwanda.
Jumla ya wanafunzi 1962 walihitimu mafunzo mbalimbali katika ngazi tofautitofauti ikiwemo stashahada na ashahada.