Home | Terms & Conditions | Help

November 28, 2024, 11:44 am

NEWS: UKATILI KWA WANAWAKE WAITESA DODOMA.

DODOMA: Imeelezwa kuwa asilimia 51 ya wanawake katika mkoa wa Dodoma wanafanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo ukeketaji.

Hayo yamesemwa na Mkurungenzi wa shirika la afnet Sara Mwaga wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Dodoma.

Mwaga amesema mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa mitano ambayo inaongoza kwa ukatili wa majumbani na ndoa za utotoni.

Awali akizungumza kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa Deograturs Yinza amesema ili kukomesha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ni lazima kuimarisha na kuboresba hali ya maisha ya kila kaya kwa kuwawezesha wanaume na wanawake ,wasichana na wavulana katika kutambua na kuzifanyia kazi fursa za kijamii na kiuchumi, kuendeleza na kuimarisha Mila,desturi imani na mitazamo inayowawezesha na kuimarisha wanawake .

Aidha ameongeza kuwa mikakati mingine ni kujenga mazingira salama na yanayotoa nafasi kwa wanawake na watoto kushiriki kikamilifu katika nyanja zote na kujenga mfumo madhubuti na shirikishi wa uratibu na upashanaji habari unaowezesha mchakato wa utoaji maamuzi sahihi katika kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Amesema katika maadhimisho hayo mambo yatakatofanyika ni kutoa Elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia kupitia vipindi vya redio kwa kutumia redio zilizopo hapa mkoani, kutoa Elimu kupitia gari maalumu la matangazo na kutoa Elimu kupitia kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanaharakati , dawati la kijinsia la polisi.

Naye msemaji wa shirika la action aid Joram Wimmo amesema njia wanayotumia kama shirika kupinga vitendo hivi ni kutoa Elimu katika jamii kwa kupitia vyombo cha habari na kutembelea vijiji mbalimbali kwa kila mkoa na kuunda vikundi vya wanawake ambavyo vinasaidia kujenga ushirikiano na kutoa Elimu nchini.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni funguka ukatili dhidi ya wanawake na watoto haumwachi mtu salama chukua hatua.